Print this page
Friday, 01 July 2022 04:51

Amani ni ombi langu Featured

Written by Faith Nelima
Rate this item
(0 votes)

Sikiliza ndugu zangu, ndugu zangu niwaenzini

Yanitokayo kinywani mwangu, kutoka kwenye nafsi

Yenye hekima manenoangu, nawasihi nisikilizeni

Amani ni ombi langu, sote tuidumishe

 

Agosti tisa mewadia, sote Kwa hamu metarajia

Asifiwe yesu kenya kwanza, wanaazimio hallelujaa

Tumsifu yesu timu wajakoya, asifiwe kristo wanaprofesa

Amani ni ombi langu, sote tuidumishe

 

Upendo umoja na amani, ndio tunu za kikristo

Wakristo tupendane nawasihi, Kwa maneno na vitendo

Kwa wengine vielelezo tuweni, alivyotufundisha yesu kristo

Amani ni ombi langu, sote tuidumishe

 

Haki huinua taifa, ndivyo asemavyo ziraili

Amani na haki hazitadumishwa, tu Kwa ombi na usemi

Eti chama Fulani kikitawala, basi ndipo itaenea amani

Amani ni ombi langu, sote tuidumishe

 

Ni jukumu letu wakristo, kujitofautisha na wengine

Wadada Kwa wandugu, jamani amani tuitende

Tuzidi kuwa mwanga, Nuru ya amani tuiangaze

Amani ni ombi langu, sote tuidumishe

 

Ole ni wa taifa, Kwa sababu ya mambo ya kukosesha

Maana hayana budi, kuja mambo ya kukosesha

Lakini ole wake mtu yule, aliletaye jambo LA kukosesha

Amani ni ombi langu, sote tuidumishe

 

Ninakusihi ewe ndugu, Dua kuipiga tuzidi

Amani ya mwenyezi Mungu, itawale yetu nchi

Amani, umoja na undugu, Kwa matendo tuiendeleze nasi

Amani ni ombi langu, sote tuidumishe.

 

~ Faith Nelima

Read 640 times