Kwa wakale "chamgei" na waluhya mm "vulai"?
Ndugu zangu wamasaai, mko "sopa" natumai
Nimekuja kuwarai, tusiwe na vurumai
Kwa umoja na upendo, tuenezeni amani
Ni ujumbe ninaweka, upate Wakenya wengi
Je mwajua ni baraka, kuwa makabila mengi
Hili sitilie shaka, baraka hizi ni nyingi
Kwa umoja na upendo, tuenezeni amani
Kabila sio, lisije kututawanya
Turkana na waluo, sisi wote ni wakenya
Sitaki kuwe kilio, cha lugha kutugawanya
Kwa umoja na upendo, tuenezeni amani
Viongozi tuchague, waongoze nchi yetu chaguo
Mwenzio simchukie, tuwapende wenzetu
Vita tusizianzie, umoja ni nguvu yetu
Kwa umoja na upendo, tuenezeni amani
Baada ya uchaguzi taendelea kuishi
Nawaambia kwa wazi, kenya kamwe haiishi
Tuuwache ubaguzi, na kwa upendo tuishi
Kwa umoja na upendo tuenezeni amani
Kwani kuna haja gani? Ndugu yako kuumiza
Na utafaidi na nini, mwenzako kimcharaza
Tukiikana amani, twajitia kwa gereza
Kwa umoja na upendo, tuenezeni amani.
Si lazima mtu wetu, ama pia mtu wenu
Sisi sote kenya yetu, si yangu wala si yenu
Hakuna huyu ni wetu, jirani yako ni wenu
Kwa umoja na upendo tuenezeni Amani
Ee Mungu nguvu yetu, dumisha upendo wetu
Na hii amani yetu, iwe hifadhi ya kwetu
Tutunze kilichochetu, migogoro siwe yetu.
Kwa umoja na upendo, tuenezeni amani
~ Faith weru
Almaarufu mchele wa chenga
Watu wa nyumba "muriega" na wakamba "mwasyata"?
Wenzangu wa kakamega, ndugu zangu wataita
Wazee pia wachanga, hatuyataki matata
Kwa umoja na upendo, tuenezeni amani
Kwa wakale "chamgei" na waluhya mm "vulai"?
Ndugu zangu wamasaai, mko "sopa" natumai
Nimekuja kuwarai, tusiwe na vurumai
Kwa umoja na upendo, tuenezeni amani
Ni ujumbe ninaweka, upate wakenya wengi
Je mwajua ni baraka, kuwa makabila mengi
Hili sitilie shaka, baraka hizi ni nyingi
Kwa umoja na upendo, tuenezeni amani
Kabila sio, lisije kututawanya
Turkana na waluo, sisi wote ni wakenya
Sitaki kuwe kilio, cha lugha kutugawanya
Kwa umoja na upendo, tuenezeni amani
Viongozi tuchague, waongoze nchi yetu chaguo
Mwenzio simchukie, tuwapende wenzetu
Vita tusizianzie, umoja ni nguvu yetu
Kwa umoja na upendo, tuenezeni amani
Baada ya uchaguzi taendelea kuishi
Nawaambia kwa wazi, kenya kamwe haiishi
Tuuwache ubaguzi, na kwa upendo tuishi
Kwa umoja na upendo tuenezeni amani
Eneza Amani

Faith weru
Almaarufu mchele wa chenga